Koffi apagawisha mashabiki wake
MWANAMUZIKI nguli Afrika, Koffi Charles Olomide alikonga nyoyo
za mashabiki wake kwenye uzinduzi wa tamasha la ‘Tusker Cannival’
lililofanyika usiku wa kuamkia jana kwenye Viwanja vya Leaders Club, Dar
es Salaam.
Koffi alipanda jukwaani saa saba kasorobo usiku baada ya onyesho la ufunguzi zilizofanywa na bendi mbalimbali za hapa nchini.
Katika onyesho hilo lililofanywa na watu 26
akiwamo Koffi, ilikuwa yenye ubunifu mkubwa huku mwanamuziki huyo
akielezea furaha yake kuweza kufika Tanzania kwa mara nyingine baada ya
miaka kadhaa aliyowahi kutembelea hapa nchini.
“Nina muda mrefu kidogo sijawahi kufika Tanzania,
naipenda nchi hii na nawapenda wote siwezi kusema ni namna gani
nimefurahi kwani niliwakumbuka,” alisikika Koffi kabla ya kuanza onyesho
hilo.
Onyesho hilo ilifunguliwa na Wazee Sugu na baadaye walifuatia Mapacha Watatu, Twanga Pepeta, Diamond Sound, Skylight Band.
Mke wa Olomide, Cindy aliimba wimbo mmoja na
kumkaribisha Koffi jukwaani, na mara alipopanda jukwaa alipokelewa na
shangwe nyingi ambazo zilidhihirisha kuwa mwanamuziki huyo bado yupo
katika chati za muziki wa dansi Afrika.
Koffi mwenye nyimbo 281, aliwataka mashabiki wa
wake wachague ni wimbo upi wanautaka kulingana na muda wake mchache
jukwaani, hali iliyokuwa ngumu kwa mashabiki waliokusanyika uwanjani
hapo kutoa majibu sahihi

No comments:
Post a Comment