Saturday, July 19, 2014

Mbunge wa viti maalumu CCM, mheshimiwa Ritta Kabati atekeleza ahadi zake


Pichani :Mheshimiwa Ritta Kabati akiwa na wadau wa shule ya msingi sabasaba.


Mheshimiwa Ritta Kabati akikabidhi mifuko ya simenti na ndoo za rangi.



Mheshimiwa Ritta Kabati kwnye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Sabasaba


Mheshimiwa Ritta Kabati akiambatana na Kamati ya ulinzi ya usalama ya mkoa watembelea Ugwachanya kutoa salaam za pole kwa wafiwa na kufika eneo liliopata ajali











Ukawa washikilia msimamo wao

Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakijadiliana jambo. 

Dar es Salaam. Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umeshikilia msimamo wake kuwa uko tayari kufanya mazungumzo ya kumaliza mpasuko uliojitokeza katika Bunge Maalumu la Katiba na siyo kurudi bungeni.
Pia umesema kwamba hawatashiriki Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 endapo Katiba Mpya haitapatikana au iliyopo haitafanyiwa marekebisho.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Ukawa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa Kamati Kuu ya Chama hicho.
“Ukawa hatuwezi kukataa mazungumzo ya kutafuta mwafaka na faida kwa Watanzania lakini tunaweza kukataa kurudi bungeni endapo kile kilichotufikisha hapa na nini kilisababisha hakijapata ufumbuzi.
Mbowe alisema Rais Jakaya Kikwete kwa mujibu wa sheria ndiye mwenye uwezo wa kuufanya mchakato huu ukamalizika salama na ikapatikana Katiba yenye kujali masilahi ya wananchi wote.
“Tunamtaka Rais (Kikwete) tunakwenda katika majadiliano aache kuwa kigeugeu na asimame kama kiongozi wa wananchi ili amalize uongozi wake salama na kuiacha nchi katika amani kama alivyoikuta,” alisema Mbowe.
Hivi karibuni katika mahojiano maalumu na gazeti hili, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema Ukawa wako tayari kurejea bungeni hata usiku wa manane endapo watahakikishiwa kuwa mjadala wa Bunge hilo utajikita katika rasimu iliyopo mezani.
“Sisi Ukawa tuko tayari kurejea bungeni hata saa nane za usiku ila wakituhakikishia tunakwenda kujadili Rasimu iliyobeba maoni ya Watanzania kinyume na hapo hatutakubali kurejea,” alisema Dk Slaa.
Alisisitiza kwamba “Hata kama tutarejea bungeni, yakitokea yaliyotufanya tutoke, tutachukua uamuzi haraka.”
Alisema CCM haina nia ya kupatikana kwa Katiba Mpya na imekuwa ikitumia nguvu kutaka kuuharibu ili Katiba hii iliyopo iendelee kutumika.
“Tuna ushahidi wa sauti ya Kamati Kuu ya CCM iliyokaa hivi karibuni wakionyesha kutokuwa na dhamira ya kweli ya kuipatia nchi hii Katiba na muda utakapofika tutauweka wazi ili Watanzania wauone na wausikie,” alisema Mbowe.
Ukawa unaoundwa na vyama vya siasa vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi vilisusa na kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge Aprili 16 mwaka huu kwa madai ya kuwa zipo dalili za kutaka kuichakachua Rasimu ya Katiba iliyosheheni maoni na mapendekezo ya wananchi.

Kufuatia mpasuko huo na Agosti 5 mwaka huu Bunge hilo likitarajia kukutana kwa siku 60, Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta ameteua wajumbe 30 wa kamati ya mashauriano inayotarajia kukutana Julai 24 mwaka huu.
Kuhusu Uchaguzi Mkuu ujao mwakani, Mbowe alisema, “Kama Katiba haitapatikana na ikabaki hii hii....Hatuwezi kuingia katika uchaguzi kwa kutumia katiba ya sasa ambayo inaonyesha kuwapo kwa tume huru ya uchaguzi kumbe siyo kweli.”
Naye Mjumbe Kamati Kuu ya Chadema na aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu alisema, “tukijidanganya nchi hii ikishindwa kupata Katiba Mpya itakuwa ni upumbavu.”
Alisema: “Kilichowatokea majirani zetu Kenya kinaweza kikatokea hata hapa kwetu, busara na hekima inatakiwa itawale ili mchakato huu umalizike salama.”
Profesa Baregu alisema “Rais (Kikwete) inabidi avue koti lake la uanachama wa CCM kama Mwenyekiti ana avae joho la urais.”

Butiku aionya CCM


Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amekionya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwa kipo hatarini kupoteza madaraka katika uchaguzi mkuu ujao, iwapo kitafanya makosa na kuendekeza ubinafsi na utawala wa kiimla unaotokana na utamaduni wa rushwa na matumizi mabaya ya mali za umma.
Butiku ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alisema kuwa iwapo chama hicho kitasahau kuwa kinaiongoza nchi kwa mujibu wa Katiba ya nchi ambayo sasa Watanzania wanataka iandikwe upya na kuendelea kukumbatia maovu kinaweza kuondolewa madarakani.
Alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam, Jumatano wiki hii katika mahojiano maalumu na gazeti hili ambapo alizungumzia mambo mbalimbali.
“…Kosa moja la msingi ni CCM kusahau misingi ya Katiba ya chama chao na Katiba ya nchi. Watanzania wengi wanaikubali Katiba ya CCM na Katiba ya nchi, lakini ambayo wanasema itazamwe upya, iandikwe Katiba Mpya,” alisema Butiku.
Huku akisisitiza, Butiku alisema: “CCM wakisahau kwamba madaraka yao ni ya kikatiba, wakadhani yapo katika utawala wa kiimla unaotokana na kuimarisha utamaduni wa rushwa na matumizi mabaya ya mali na rasilimali za taifa, watapoteza madaraka kama siyo leo ni kesho.”
Alifafanua kuwa hali hiyo itaikumba CCM kwa kuwa ndiyo kanuni ya maisha ya binadamu akisema:
“Vyama vyote tawala vilivyosahau masilahi ya wananchi wake, demokrasia, uhuru na haki, vikakumbatia uovu vinaanguka. Huo siyo utabiri wangu binafsi, bali historia itawahukumu.”
Butiku alitoa mfano akieleza: “Mfumo wa kibabe zaidi wa makaburu wa Afrika Kusini, uliangushwa na wasio na viatu. Nani anaweza kujenga ubabe wa sura kama ule wa makaburu, nani ataruhusu? Ni muhimu CCM nayo ijitazame.”
Rushwa
Alisema kuwa alipoondoka madarakani, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alisema taifa linanuka rushwa hali ambayo imeota mizizi hata sasa.
“…Leo rushwa ni kawaida, ni mfumo wa kuuza na kununua uongozi, kama taifa mkifika hapo ni hatari. Mkishanunua uongozi basi mmekwisha. Mkijenga mfumo huo, mnaondoa haki.
Ikiwa kura yako imekuwa biashara umekwisha, hakuna ushirikiano tena kati ya kiongozi aliyenunua nafasi na mwananchi. Hapo mnajenga kundi la viongozi la wafanyabiashara wa kura katika uchaguzi, mnajenga mfumo wa raia kuwa maskini.”
“Raia wakiuza haki yao na kununua hakutakuwa na taifa lenye utulivu. Wanunua kura wajue ni vita, siku moja wauza kura wataamua kuwaondoa nao watagoma kwa kuwa walinunua uongozi, hapo damu itamwagika, watu watauana.
Wanyonge hawapotezi haki ya unyonge wao, unaweza kuiangusha CCM.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Monday, July 14, 2014

MAJANGA CHADEMA JIMBO LA IRINGA MJINI ,VIONGOZI WAKE KATA YA RUAHA WASEMA WAMECHOSHWA NA UBABAISHAJI WA MBUNGE MSIGWA WAREJEA CCM ,WAMPA TANO KABATI



Diwani  wa kata ya Mtwivila Vitus  Mushi akisaliama na wadau  leo.




viongozi  wa Chadema  waliohamia  CCM leo katika mkutano wa CCM kuimarisha chama uliofanyika mtaa wa Kwa mwagongo.




Aliyekuwa  katibu kata ya Ruaha  Juma Kapalampya  kushoto  akikabidhi nyaraka ya siri ya Chadema na kadi 40 kwa katibu wa CCM mkoa Hasan Mtenga  leo ,kulia ni mbunge wa  viti maalum mkoa wa Iringa Ritta kabati.
Baadhi ya  nyaraka za  Chadema na kadi





Makada  wa  Chadema  waliojiunga na CCM Iringa mjini  wakila kiapo

Chanzo:www.iringa-yetu.blogspot.com



Kampuni ya uwindaji yampinga Nyalandu, yatishia kwenda kortini

Mheshimiwa Lazalo Nyalandu
Kampuni ya Uwindaji ya Green Miles Ltd (GMS) iliyofutiwa leseni ya uwindaji imemuweka njia panda Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, baada ya kupinga uamuzi huo uliochukuliwa na waziri huyo na sasa imepanga kwenda mahakamani kudai haki kisheria.
Waziri Nyalandu alitangaza kuifutia leseni ya uwindaji nchini pamoja na shughuli za utalii kampuni hiyo kwa madai ya kukiuka sheria mbalimbali za uwindaji wanyamapori Julai 11, mwaka huu.

Mwanasheria wa kampuni hiyo, ambaye ni Wakili wa kampuni ya Uwakili ya Haki Kwanza, Alloyce Komba, akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, alisema GMS itakwenda mahakamani kama viongozi wa juu wa serikali watashindwa kushughulikia tatizo hilo.

“Iwapo mamlaka za juu za serikali hazitashughulikia jambo hili ili haki itendeke, kampuni ya GMS italazimika kwenda mahakamani kudai haki ya kurejeshewa leseni zake pamoja na kudai kulipwa fidia kutokana na hasara iliyopata baada ya kushindwa kufanya 

Alisema uamuzi huo utafikiwa baada ya kuandika barua kwenda kwa viongozi wa juu wa serikali kwa maana ya Waziri Mkuu na Katibu Mkuu Kiongozi, kwani kampuni inaamini kwamba, Waziri Nyalandu ametekeleza hilo ili kutekeleza lengo lake ovu ili aweze kukigawa kwa rafiki zake.

Komba alisema ni jambo la kusikitisha kwamba, licha ya kampuni hiyo kufanya uwekezaji mkubwa na kulipa ada zote za serikali, imejikuta ikihujumiwa na waziri aliyepewa dhamana ya kusimamia sekta ya maliasili ya utalii kwa ajili ya kulinda maslahi ya kampuni ya kigeni.

Alisema kampuni ya GMS haikupewa nafasi ya kujitetea na badala yake Waziri Nyalandu aliamua kutoa maamuzi ya kuifutia leseni na siku chache baada ya kufanya hivyo ameondoka nchini na kwenda Marekani ambako yapo makao makuu ya kampuni moja ambayo ina mgogoro na kampuni ya GMS. 

Julai 11 mwaka huu, Waziri Nyalandu alisitisha kibali cha umiliki wa kitalu kwa kampuni hiyo kufuatia madai ya uwindaji usiozingatia sheria ya uhifadhi wa wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 kama ambavyo pia ushahidi huo ulielezwa kuthibitishwa kupitia DVD hiyo.

Makilagi:Bila Ukawa hakuna Katiba mpya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Amina Makilagi, amesema bila kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kurejea bungeni na kushiriki katika hatua zote zilizobaki, Katiba mpya ya Tanzania ni ndoto kupatikana.
Katibu huyo aliyasema hayo mwishoni mwa wiki kwa nyakati tofauti mbele ya viongozi wa CCM na mikutano ya hadhara katika vijiji vya Iyogelo, kata ya Binza, Kizungu kata ya Sayusayu, wilayani Maswa, akiwa katika ziara ya kikazi wilayani hapa, mkoa wa Simiyu.
Alisema ili Katiba mpya ipatikane ni lazima kundi la wajumbe wanaounda kundi la Ukawa waliosusia vikao vya bunge hilo wakarejea.

Makilagi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, aliwaomba wanachama na wananchi kuwaombea Ukawa kwa Mungu ili waweze kurejea Bungeni Katiba mpya ipatikane.

“Hatuwezi kuunda Katiba mpya bila hawa wenzetu waliosusia Bunge Maalum la Katiba kurejea bungeni, hivyo tunaomba sana mtuombee wananchi hasa tunapoelekea katika Bunge hilo mwezi ujao” alisema.

Alisema kukwama kwa mchakato huo kutatokana na kutofikiwa kwa idadi ya wajumbe katika upigaji kura ili kupata theluthi mbili za uamuzi wa vikao vya Bunge hilo kwa mujibu wa kanuni zilizopo.

Kauli hiyo imekuja huku juhudi za watendaji wa Bunge na makundi mbalimbali katika jamii wakiwamo viongozi wa dini kuwasihi Ukawa kurejea bungeni zikiendelea.

Kuhusu chaguzi zijazo, Katibu Mkuu huyo wa UWT, alitaka vijana kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi katika chaguzi zijazo za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani.


Chanzo:www.ippmedia.com

Ridhiwani apendekeza 11 wanaofaa kuwa Rais


Dar es Salaam. Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete ametaja majina 11 ya wanachama wa CCM wanaofaa kuwania urais kurithi kiti cha baba yake, Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda wake mwakani.
Ridhiwani (35), ambaye alishinda kiti cha ubunge wa Jimbo la Chalinze Aprili mwaka huu, alitaja majina hayo katika mahojiano maalumu na gazeti hili yaliyofanyika mjini Dodoma hivi karibuni.
Miongoni mwa aliowataja kuwa wana sifa ni makada watano walio chini ya uangalizi wa CCM wa mwaka mmoja baada ya kubainika kuanza kampeni za urais mapema, mawaziri wawili waliopoteza nyadhifa zao katika kashfa ya Operesheni Tokomeza, mwanamke mmoja na Rais wa Zanzibar.
“Kutaja majina tu, naweza kuorodhesha wengi tu. Naweza kuorodhesha hata watu 500, kwa sababu tunaona wengi sana,” alisema mtoto huyo wa Rais Kikwete ambaye amekuwa ndani ya CCM kwa muda mrefu akitokea umoja wa vijana wa chama hicho, UVCCM. “Kwa mfano, kwa upande wa Bara tunao Emmanuel Nchimbi, William Ngeleja, January Makamba, Bernard Membe, Steven Wassira, Edward Lowassa na Asha-Rose Migiro,” alisema.
Aliongeza: “Hawa ni kwa uchache zaidi… ni baadhi ya watu ambao wanatajwa kwa upande wa Bara, lakini jambo la msingi ni nani mwenye sifa za kuwa rais.”
Alisema pamoja na kwamba wanasiasa hao wote wanazo sifa za kuiwania nafasi hiyo ya juu, vikao vya chama ndivyo vitakuwa na nafasi ya kuwachuja ili kupata wanaotosha. “Kama wanatosha au la, vikao vya chama vitakaa kuamua licha ya kuwa hao wote niliowataja, kwa sifa za kugombea urais wote wanajitosheleza. Wana sifa, wana uwezo wa kugombea na wana uwezo wa kushinda, hao ni kwa upande wa Bara,” alisema.
Alipoulizwa hali ikoje kwa upande wa Zanzibar, Ridhiwani alisema, “Sisi chama chetu kina utajiri wa watu kwa upande wa Zanzibar kuna Shamsi Vuai Nahodha, Hussein Ali Mwinyi, Dk Seif Ally Iddi (Makamu wa pili wa Rais Zanzibar) na Dk Mohammed Ali Shein, Rais wa Zanzibar. Hawa ni watu ambao wana uwezo na hata wakipewa jukumu la kuongoza nchi hii wanaweza. Tunao wengi sana.”
Membe, Wassira, Lowassa, Ngeleja na Makamba walipewa adhabu na Kamati ya Maadili ya CCM ya kutogombea nafasi yoyote ndani ya chama wala kufanya kampeni baada ya kudaiwa kukiuka taratibu za chama hicho, wakati Nchimbi na Nahodha walilazimika kujiuzulu nyadhifa zao za uwaziri kutokana na kashfa ya Operesheni Tokomeza ambayo ililenga kushughulikia majangili, lakini ikahusishwa na vitendo vya ukiukaji haki za binadamu.
Ridhiwani hakumtaja Waziri Mkuu wa zamani, Fredrick Sumaye ambaye pia anatumikia adhabu hiyo ya Kamati ya Maadili ya CCM.
Baadhi kukwama
Hata hivyo, Ridhiwani alidokeza kuwa wapo baadhi ya wanasiasa watakaokwama kufikia lengo hilo kutokana na kukabiliwa na kesi ndani ya chama, ambazo hakuzitaja wala kutaja wahusika.
“Kuna watakaopungua kutokana na kesi zinazowakabili katika chama ambazo zinawafanya wapungukiwe sifa. Kwa maana hiyo kuna watu kama wanne hivi (wa Bara) unawatoa na ukiwatoa unabakiwa na watatu, sasa unaweza kujiuliza hao watakaobaki watatu, je, wanatosha?”

Chanzo:www.mwananchi.co.tz