Katibu huyo aliyasema hayo mwishoni mwa wiki kwa nyakati tofauti mbele ya viongozi wa CCM na mikutano ya hadhara katika vijiji vya Iyogelo, kata ya Binza, Kizungu kata ya Sayusayu, wilayani Maswa, akiwa katika ziara ya kikazi wilayani hapa, mkoa wa Simiyu.
Alisema ili Katiba mpya ipatikane ni lazima kundi la wajumbe wanaounda kundi la Ukawa waliosusia vikao vya bunge hilo wakarejea.
Makilagi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, aliwaomba wanachama na wananchi kuwaombea Ukawa kwa Mungu ili waweze kurejea Bungeni Katiba mpya ipatikane.
“Hatuwezi kuunda Katiba mpya bila hawa wenzetu waliosusia Bunge Maalum la Katiba kurejea bungeni, hivyo tunaomba sana mtuombee wananchi hasa tunapoelekea katika Bunge hilo mwezi ujao” alisema.
Alisema kukwama kwa mchakato huo kutatokana na kutofikiwa kwa idadi ya wajumbe katika upigaji kura ili kupata theluthi mbili za uamuzi wa vikao vya Bunge hilo kwa mujibu wa kanuni zilizopo.
Kauli hiyo imekuja huku juhudi za watendaji wa Bunge na makundi mbalimbali katika jamii wakiwamo viongozi wa dini kuwasihi Ukawa kurejea bungeni zikiendelea.
Kuhusu chaguzi zijazo, Katibu Mkuu huyo wa UWT, alitaka vijana kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi katika chaguzi zijazo za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani.
Chanzo:www.ippmedia.com
No comments:
Post a Comment